
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter amempongeza Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa kuchaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu na kumuahidi ushirikiano zaidi.
Wanyarwanda walipiga kura jana August 4, 2017 ambapo Rais Kagame kupitia tiketi ya chama cha FPR ametangazwa mshindi wa kiti hicho kwa asilimia 98.
