Quantcast
Channel: TANZANIA CLASSIC
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5823

HUYU NDIO NYOKA MWENYE KASI ZAIDI NA MWENYE SUMU KALI ZAIDI DUNIANI

$
0
0
 imeandikwa  na  Josephat K. Nyambeya  kupitia  ukurasa  wake  wa  facebook
Image may contain: outdoor
HUYU NDIO NYOKA MWENYE KASI ZAIDI NA MWENYE SUMU KALI ZAIDI DUNIANI

Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya Kingereza huitwa Black Mamba.

MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo. Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).

Kuna aina mbili za mambas :
1. GREEN MAMBAS.
2. BLACK MAMBAS.

Green mamba wana sumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC. Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.

BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320. Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika. Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.

Mambas ni nyoka wakali na wenye kung'ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang'ooki wakti wakigonga kitu. Meno yanayong'ooka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong'ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.

BLACK MAMBA. 

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. 
Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.

1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na Kilo 1.58757 katika uzito. 

2- Black mamba ana mwili mwembamba wenye kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini wengi hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano. 

3- Black mamba ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba huonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari. 

4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio. 

Ukiona ameonyesha moja ya hizo ishara unashauriwa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwahi kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee, narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake. 

5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini na yeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae.

6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza huua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua. 

7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake.

8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere. 

9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 sawa na Kilomita 20 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako. 

10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.

11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.

12. Nyoka huyu ana akili sana, anakula sana majani ya bangi, na mara nyingi hupenda kukaa kwenye mashamba ya bangi mida ya mchana, mara nyingi ana ng'ata kichwa na shingo tu, ana wika kama jogoo kwa hiyo jihadhari sana ukiwa porini na ukasikia mlio wa sauti kama ya jogoo. Hajawahi kutembeea kichwa chini yaani siku zote kichwa chake kipo juu kama kasimama vile. Ana kwepa sana mawe, ana ruka kama panzi. 

13. Iwapo nyoka huyu atakung'ata utaweza kuishi hadi dakika 20 tu.

14. Akikomaa zaidi anakuwa na ukucha kwenye mkia. Pia akikomaa zaidi magamba yake huwa yanatoa sauti akikimbia kwa sauti inakuwa kama chupa inayovunjika. 

14. Kwa Tanzania wanapatikana sana mikoa ya Singida, Tabora, Dodoma, Katavi na kule kwetu Mara pia wapo na mikoa ya kanda ya ziwa, na kanda ya kusini. 

Ukikutana naye akiwa amesimama mbele yako usijaribu ujanja wowote hutaweza kumuwahi, labda umwombe Mungu akupe ujasiri wa kutulia tuli hadi ashushe kichwa chini ndio ujaribu ujanja mwingine otherwise WAFWA, akikuuma kichwani sijui utafunga wapi. 

GREEN MAMBA.

Green mambas wqnapenda sana kuishi karibu na maji hasa mito! Mara nyingi sana hupendelea kukaa kwenye miti ya kijani kwa ajili ya mawindo sana sana hupenda kukamata ndege ! Nii vigumu sana kumwona kulingana na rangi yake!!! Usipokuwa makini anaweza hata kukunga 'ata kichwa/shingo ,na hukawii kufa!

Usisite kutembelea page yetu ya Teknolojia Kwanza kwa mafunzo na maandiko zaidi ya kufungua ufahamu.


TANGAZO,  #TANGAZO #TANGAZO

  KUTOKA MTANDAO HUU

Image may contain: 1 person, smiling, text

Mtandao  wa kijamii  wa   www.tanzaniaclassic.com   {THE  GIANT SOCIAL MEDIA IN EAST AFRIKA}  unakuletea  shindano  la ADVERTISING  BUSINESS COMPETITION .

ADVERTISING   BUSINESS  COMPETITION –Ni  shindano   ambalo  linatoa  fursa  kwa wafanyabiashara au  wajasiriamali kutengeneza Tangazo  nzuri la  biashara  zao  lenye  ubunifu,  Matangazo hayo yatawekwa  kwenye  mtandao  wa  www.tanzaniaclassic.com  ili  kusaidia wafanyabiashara na wajasiriamali kutangaza  biashara  zao  kwa   gharama  nafuu  sana,  Pia  matangazo hayo yatashindanishwa  kutafuta tangazo  bora  lenye  ubunifu  ambapo  mshindi  wa  kwanza  atazawadiwa  shilingi  500,000  na  nafasi ya  kutangaza biashara  yake  bure kwenye  mtandao  wa www.tanzaniaclassic.com  kwa  miezi sita.

Pia  mtandao wa www.tanzaniaclassic.com  utatoa  ofa  kwa  mshindi   ya  kumsaidia  kubrand biashara yake ili  iweze  kujulikana Zaidi  na kupata  soko ndani ya Afrika  mashariki.

Mshidi  atapata fursa  ya  kukutanishwa  na wajasiriamali na wafanyabiashara waliofanikiwa  zaidi   ili  aweze  kupata uzoefu zaidi  ...       

Mshiriki  wa  ADVERTISING  BUSINESS  COMPETITON  ambaye   ni  mfanyabiashara au  mjasiramali  anatakiwa  kutengeneza    tangazo  lenye  mvuto  na ubunifu  juu  ya biashara  anayofanya   ili  ajiweke  kwenye  nafasi  nzuri  ya  kushinda..

 Mshindi  wa  ADVERTISING   BUSINESS  COMPETITION  Atachaguliwa  na  majaji  wa www.tanzaniaclassic.com  baada  ya  kupitia  matangazo  yote  ambayo  yatakuwa  yameingia  kwenye shindano  hili, Vigezo vikuu mpaka  mshindi apatikane  itakuwa  ubunifu  wa tangazo  husika, Ubunifu wa  lugha  katika  tangazo husika , mwenekano  mzuri  wa tangazo  nk.

Shindano  la ADVERTISING  BUSINESS  COMPETITION  ni shindano  ambalo  linahusisha  hasa wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka   Tanzania  na Kenya ambapo   mtandao wa www.Tanzaniaclassic.com  una watembeleaji wengi zaidi,Pia wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka  nchi zingine  za  ukanda Afrika  mashariki ambao watependa kushiriki shindano hili wataruhusiwa kushriki..

MASHARTI NA  VIGEZO VYA  KUSHIRIKI  ADVERTISING  BUSINESS COMPETITION

1.Mshiriki anatakiwa awe  na  umri wa miaka  18 na  kuendelea,,

 2.Mshiriki wa  ADVERTISING  BUSINESS COMPETITION anatakiwa  analipie  tangazo  lake  kwanza kwa  shilingi  elfu  50,00 0 ndiyo  litapata  fursa  kurushwa  kwenye  www.tanzaniaclassic.com  pamoja  kuingia  kwenye   shindano la  ADVERTISING BUSINESS  COMPETITION 

2.Mshiriki  anatakiwa  atoe  tangazo  la  biashara  inayofanyika  tayari  na  inaendelea  kufanyika  wakati      

4.Mshiriki wa  ADVERTISING S COMPETITION  harusiwi  kukopi  tangazo  la  mshiriki mwingine  ambayo  yatakuwa  yanarushwa  na  www.tanzaniaclassic.com  wakati  shindano  likiendelea .

5.Wafanyakazi  na ndugu  ambao wanaohusiano  na  mtandao  wa www.tanzaniaclassic.com  hawataruhusiwa  kushiriki  shindano hili..

6.Mshiriki  anaruhusiwa  kuingiza  matangazo     yasiyozidi  3  kwenye  shindano  lakini  lazima  hayo  matangazo  yawe  ni ya biashara  tofauti  ambazo  zinafanyika  na zinaendelea wakati huo.  

        FAIDA  ZA  KUSHIRIKI  ADVERTISING  BUSINESS  COMPETITION 

1.Shindano  la  ADVERTISING BUSINESS COMPETITION  linatoa   fursa  wafanyabiashara  na wajasiriamali  kutangaza  biashara zao kwa kipindi cha  miezi  2  na nusu    wakati  wa shindano likiendelea.     

2.Shindano la  ADVERTISING  BUSINESS  COMPITETION   litasaidia  sana wafanyabiashara  na wajasiriamali  biashara  zao  kujulikana pamoja na biashara zao  kupata  soko  kutokana  na  mtandao wa www.tanzaniaclassic.com  kutembelewa  na watu  wengi ndani na  nje  ya Afrika  mashariki .

3.Shindano la  ADVERTISING  BUSINESS  COMPETETION   litasaidia  kutoa  hamasa  kwa wafanyabiashara  na  Wajasiriamali  kuwa  wabunifu na  wadadisi katika kuandaa   matangazo  yanayohusu  biashara  zao  ambayo yatasaidia  biashara  zao  kujulikana   na  kupata  masoko  Zaidi .

  Shindano  hili  litaanza tarehe   12-8-2017  Mpaka  tarehe  29-10-2017 

  Jinsi ya  kushiriki  shinadno  la  ADVERTISING BUSINESS COMPETITION.

   Wasiliana na  sisi kupitia   simu : +255655515906

                                                 Whatsapp: +255755515906

                                                 Email :tanzaniaclassic1@gmail.com     

   Fika  ofisini  kwetu:               Msasani,Macho   

                                                              Dar-Es-Salaam

  Kwa kufatilia shindano la  ADVERTING  BUSINESS COMPETITION   endelea kutembelea  mtandao wa  www.tanzaniaclassi.com

  Facebook;    Tanzaniaclassic  media

   Instagram: Tanzaniaclassic media       

  You tube:Tanzania classic  




Viewing all articles
Browse latest Browse all 5823