Quantcast
Channel: TANZANIA CLASSIC
Viewing all 5823 articles
Browse latest View live

Mwanafunzi wa Chuo Cha IFM afikishwa Mahakamani kwa kumwingiza mtoto vidole sehemu za siri

$
0
0
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mussa Msafiri (23), alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jana akituhumiwa kumwingizia vidole sehemu za siri mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Mbele ya Hakimu Issa Kasailo, Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande, alidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 7 mwaka huu maeneo ya Sinza alikokuwa anaishi mwanafunzi huyo.

“Mtuhumiwa ulitenda kosa hilo wakati ukitambua kwamba ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai wakili.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na upelelezi unaendelea.

Hakimu Kasailo alisema shitaka hilo linadhaminika hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaoweka saini ya maandishi ya Sh milioni tano kwa kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Febuari 27 mwaka huu na mtuhumiwa aliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.


Amuua Mwenzake Kwa Kipigo Baada ya Kumkuta Akimtongoza Dada Yake

$
0
0


Mkazi wa kijiji cha Kalovya – Inyonga wilayani Mlele, Ramadhani Ally (20) amefariki dunia akipatiwa matibabu hospitalini baada kupigwa na kijana mwenzake.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari amesema kuwa Ramadhani alifikwa na umauti baada ya kujeruhiwa na kijana mwenzake Ntema Kabembenya( 26), mkazi wa kijiji cha Ipwaga.

Kidavashari amesema tukio hilo lilitokea Januari 22, mwaka huu saa 12:55 jioni ambapo Ntema alimkuta Ramadhani (marehemu) akimtongoza dada yake (Ntemwa) mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa).

“Ntemwa alikasirishwa na kitendo cha Ramadhani kumtongoza dada yake mwenye umri wa miaka 12, alimshambulia Ramadhani kwa kumpiga na fimbo na kumjeruhi vibaya,” alieleza Kamanda Kidavashari.

Inadaiwa Ramadhani alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Mlele kwa matibabu lakini alifariki dunia siku iliyofuata akiwa anatibiwa.

Kwa mujibu wa Kidavashari, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.

SOMA UJUMBE WA LEO HAPA

NGUVU KUBWA IMETUMIKA BUNGENI!!!!! ,SOMA HAPA KUJUA UKWELI

$
0
0


Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima aliyeko katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma, ameripoti kupitia DW (Kiswahili) kuwa, waandishi wa habari na wapiga picha, 'picha mnato' (still pictures) na 'picha za kutembea' (moving camera), wamezuiwa kutekeleza majukumu yao wakati vurugu zilipotokea Bungeni jioni hii.
Ameeleza kuwa kuna mbunge amevuliwa koti, viatu na soksi na kubakishwa na suruali na 'singland' pekee huku wabunge wanawake wakidhalilishwa na vyombo vya dola waliotumia nguvu kubwa kuwatoa ukumbini, baadhi wamesikika wakipiga kelele za kudhalilishwa na kupoteza vito vyao vya thamani ikiwemo mikufu, hereni, bangili na pete za dhahabu, mbwa wa polisi walifika katikati ya lango kuu la kuingilia ndani ya ukumbi wa Bunge kitu ambacho si chakawaida.
Inaarifiwa kuwa, wakati wakitolewa nje ya ukumbi walipata mkong'oto mkali huku matukio hayo yakishindwa kurekodiwa kwa sababu waandishi walidhibitiwa ipasavyo, na kutakiwa kuondoka kabisa eneo la tukio pasipo kuchukuwa picha ya matukio hayo.
Askari wa kiume wametumika kuwatoa nje wabunge wa kike kitu ambacho kimatajwa kuwa ni udhalilishaji uliovuka mipaka, askari wapato 30 waliovalia mavazi rasmi ya kiaskari, askari wa Bunge, Usalama wa Taifa na askari kanzu waliingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kutumia nguvu kuwatoa wabunge wa upinzani.
Bunge linaendelea kujadili hoja ya Waziri Mkuu kuhusu hotuba ya Rais aliyoitoa Novemba 20 mwaka jana huku likiwa na wabunge wa chama tawala pekee, wabunge wote wa upinzani akiwemo Zitto Kabwewamekutana katika kikao cha dharura kujadili hali hiyo na utatuzi wake.



KWA  HISANI    

Ally Mohammed

Serikali Yasema Mawaziri Wakuu Waliokihama Chama cha Mapinduzi (LOWASSA na SUMAYE ) Wataendelea Kulipwa Pensheni Zao Kama Kawaida

$
0
0

Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.


Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba.

Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.

Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni itakayokidhi mahitaji yao.

Habari kubwa leo !!!! Cuf kutoshiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar. leo!!!

$
0
0
Baraza kuu la chama cha CUF chini ya mwenyekiti wake wa muda wametangaza kutokushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar.


AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali. Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.

2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

3. KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.

4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.

5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.

6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke. Baraza Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.

8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar. Baraza Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.

9. KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.

10. KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.

11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani. Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.

12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.

LIMETOLEWA NA:
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016

Sakata la Bunge Kutokuonyeshwa Laivu Lawapatanisha Zitto Kabwe na Mbowe...Wapeana Mikono na Kukaa Pamoja

$
0
0

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kulia) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakipinga kitendo cha kutolewa kwa nguvu katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. 
March 10 2015, Zitto Kabwe alivuliwa uanachama wa CHADEMA  kwa tuhuma za kukihujumu na kikisaliti chama hicho.
Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Zitto alijiunga na chama cha ACT-Wazalendo na kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho huku mwenyekiti wake akiwa Anna Mghwira


Dr: MWAKA : NIMESOMA NA NINA TAALUMA ,ASIYETAKA AJE TUPIMANE.

$
0
0

Kwa Mara ya kwanza tangu akumbwe na 'sekeseke' la ziara ya kushtukiza na Serikali katika kituo chake cha tiba mbadala, Tabibu J.J Mwaka amezungumza na Times FM kufafanua tukio hilo.
Akizungumza kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM, Mwaka amesema Uwezo wake kitaaluma hauna shaka kwani amesomea nchini China na ndio maana Serikali imempa usajili kwa kutambua uwezo wake.
"Taaluma yangu haina mushkeri, ukizungumzia China ndio inaongoza kwa Tiba asili duniani, nimesoma kule na hili halina shaka" alisema.
"Nimesoma Nina taaluma, asiyetaka aje tupimane uwezo" ameongeza.
Akijibu swali lililoulizwa na Mtangazaji Mariam Kitosi kuhusiana na kuvunja sheria kwa kujiita DAKTARI, Tabibu huyo amedai haoni tatizo kuuitwa hivyo na hato acha kujiita Dr kwa kuwa ni katika matumizi tu ya Lugha.
"Ukisema Tabibu ni Kiarabu, ambapo kiswahili ni Mganga, na kingereza ni Dr. Tatizo likowapi?"
Akifafanua kuhusu kumkimbia Naibu Waziri wa Afya Dr Hamis Kigwangala, kwa kuruka ukuta ofisini kwake Fore Plan Clinic, Mwaka amesema ni walipishana tu kwa kuwa hakuwa na taarifa ya ujio wa Waziri huyo.
"Mchapakazi anamjua mchapakazi mwenzie, alipata feelings kama hizo (kukimbiwa), ukweli nilitoka kabla hajafika na sikuwa na taarifa kama angefika" Alisema.

Serikali: Tutawafilisi Mafisadi na Wahujumu Uchumi

$
0
0


Serikali kupitia vyombo vyake vya dola, imetangaza kuzitaifisha mali za wote waliopatikana na hatia ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi na kueleza kuwa utaratibu huo ndio utakaoendelea kwa watuhumiwa ambao bado kesi zao hazijamalizika au hazijapelekwa mahakamani.

Tangazo hilo la serikali limetolewa leo Januari 28, 2016 na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, DPP, Bw. Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi(DCI), Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani na Mkurugenzi wa Upeleelzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wakati wa mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha kuwa jukumu hilo linatekelezwa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai amesema, mwaka 2012 idara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa pamoja walikubaliana kufanya kazi ya ufuatiliaji wa mali zinazohusiana na uhalifu kama sheria inavyotaka na kwa upande wa jeshi hilo tayari kitengo chake cha upelelezi wa makosa ya uhalifu wa kifedha (Money laundering) kiko kazini.

“Katika kutekeleza mkakatihuo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ha hizo ,kesi tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya Mahakama ili ziweze kuzuiwa au kutaifishwa (Restraint or confiscation).” Alifafanua Kamishna Diwani Athumani

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi kutoka TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo, yeye amesema, taasisi yake imeona hakuna maana yoyote kwa mhalifu wa Ufisadi na uhujumu uchumi ukamfunga gerezani na kisha kumuachia baada ya kifungo halafu aendelee kutumia mali alizochuma kwa njia za haramu.

“Tumeona njia mbadala ya kudhibiti hali hiyo na kwa mujibu wa sheria ni kumfilisi mhusika hata kama atatumikia kifungo.” Alibainisha Bw. Alex

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP, Bw. Biswalo Mganga, yeye amesema ili kuendana na dhana ya Hapa Kazi Tu, ni lazima kukabiliana na wahujumu uchumi na Mafisadi ili hatimaye Wananchi walio wengi waweze kunufaika na rasilimali zao. 

“Natoa wito kwa nyie waandishi wa habari muujulishe umma wa Watanzania kuwa kama mtu anayo taarifa au anajua mali zinazomilikiwa na mtu isivyo halali hususan watumishi wa umma basi atoe taarifa.” Alisema

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA KUTOKA TANZANIA CLASSIC

$
0
0
                                                    /DSC00508
  DSC00492DSC00508 DSC00493 DSC00494 DSC00495 DSC00496 DSC00497 DSC00498 DSC00499 DSC00500 DSC00501
DSC00502 DSC00503 DSC00504 DSC00505 DSC00506 DSC00507 DSC00508 DSC00509 DSC00510 DSC00511
DSC00512 DSC00513 DSC00514 DSC00515 DSC00516 DSC00517
DSC00518 DSC00519 DSC00520 DSC00521 

Serikali Yatoa Tamka Kuhusu Kuruhusiwa TV Binafsi Kurusha Matangazo ya Bunge Laivu

$
0
0



Wakati Bunge likieleza kuwa haliwezi kuzuia vituo vya televisheni nchini kuonyesha moja kwa moja matangazo ya shughuli za vikao vya Bunge, Serikali imetoa sababu tatu za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupunguza matangazo hayo ya shughuli za chombo hicho chenye mamlaka ya kutunga sheria.

Uamuzi wa Serikali kuhusu TBC ulizua sintofahamu bungeni na kusababisha polisi kutumika kuwatoa katika Ukumbi wa Bunge, wabunge wa upinzani waliokuwa wakishinikiza kusitishwa kwa mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli, badala yake lijadiliwe suala hilo la shirika hilo.

Naibu Katibu wa Bunge, John Joel alisema jana kuwa hakuna televisheni yenye mkataba na Bunge kurusha moja kwa moja matangazo hayo, zote zinazorusha zinatumia gharama zao wenyewe.

Baada ya TBC kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge, televisheni zilizobaki ambazo zinarusha moja kwa moja matangazo hayo, ni Star TV kupitia chaneli yake ya Star Bunge pamoja na Azam TV.

 “Sisi hatuna mkataba nao, wao wanarusha kwa gharama zao na Bunge haliwezi kuwazuia, labda waulizwe wenyewe kama wataendelea kurusha matangazo hayo ama laa,” alisema Joel huku akisisitiza kuwa hakuna zuio lolote.

Juzi jioni Waziri wa Habari, Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kueleza sababu tatu za kupunguzwa kwa matangazo hayo.

Nape aliitaja sababu ya kwanza kuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji, “Kwa mwaka TBC ilikuwa inatumia Sh4.2 bilioni kurusha moja kwa moja matangazo haya. Fedha hizi hazilipwi na Bunge wala Serikali, zinatokana na matangazo madogo ya TBC, sasa pia hesabu tangu 2005 mpaka sasa zimetumika kiasi gasi.”

Alisema sababu nyingine ya kupunguza kurushwa kwa Bunge ni kutaka wafanyakazi wa Serikali kufanya kazi kikamilifu, kwa madai kuwa wengi badala ya kufanya kazi walikuwa wakifuatilia vipindi hivyo.

Alisema utafiti uliofanywa na Serikali umebaini kuwa waendesha bodaboda, mamalishe, wamachinga, wakulima, wafugaji na watu wenye shughuli nyingi wanashindwa kufuatilia vipindi vya Bunge asubuhi na mchana kutokana na kubanwa na shughuli zao.

Bunge laahirishwa ghafla, yadaiwa Serikali imekiuka taratibu za bunge

$
0
0

Wabunge wa Upinzani wasababisha bunge la asubuhi kuahirishwa hadi Jioni. Mapema baada ya Maswali na Majibu, Waziri wa Fedha Dokta Philip Mpango, alisoma Muelekeo wa mpango wa Serikali wa Maendeleo wa mwaka 2016/2017. 


Baada ya kumaliza kusoma, Zitto Kabwe na Tundu lissu, Wakaomba Muongozo wakieleza kwamba, Waziri wa Fedha amesoma muelekeo wa mpango wa maendeleo wa Mwaka mmoja badala ya miaka mitano, hivyo kavunja katiba, sheria na kanuni za Bunge.

Mwenyekiti wa Bunge alikua Andrew Chenge, akatoa mwongozo wake kwamba swala hilo atalitolea ufafanuzi baadae baada ya kukutana na Uongozi wa Bunge. 

Alivyo maliza kutoa muongozo, akamuita Msemaji wa Kambi ya Upinzani, ambapo Mh. Davidi Silinde, alisimama mbele ya bunge na kusema hawezi kusoma muelekeo wa Mpango wa maendeleo wa Mwaka 2016/2020 wakati Serikali haijasoma Mpango wake, akaitaka Serikali isome kwanza mpango wake kama kanuni na desturi ya bunge kisha Msemaji wa Upinzani afuate.

Silinde akasema sisomi, akaenda kukaa.

Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge, akaamua kuahirisha Kikao cha Bunge hadi jioni.

.: Raila WARNS Uhuru AGAINST ECONOMIC SABOTAGE of in Opposition strongholds

$
0
0

BREAKING: Raila WARNS Uhuru AGAINST ECONOMIC SABOTAGE of in Opposition strongholds
STATE MUST PROTECT LEGITIMATE BUSINESSES:
About a week ago, the Governor of the County of Mombasa Hon Ali Hassan Joho stood up against the bullying tactics being employed by the National Executive particularly to bully governors from the Opposition.
This well intended challenge to the presidency which has the backing of the Constitution, was certainly not received well by the National Executive. Revenge was sure to follow and it has.
Yesterday, the government shut down two container freight stations belonging to Governor Hassan Joho’s family.
KPA Managing Director Mr Gichiri Ndua gave no reasons for closing the facility. It was done through executive fiat.
This development would not be so worrying if it were not for its echoes of a return of an old order Kenyans are only too familiar with.
This is not about the governor and his businesses. It is about the return of strong arm politics, intimidation and blackmail to fight the Opposition, individuals and communities into surrender.
It is a return of the old order of starving individuals and communities into submission and surrender.
It has sad echoes of the1970s and 1980s when businesses were deregistered, slapped with hefty taxes and shut down because the owners were perceived to be anti government or unwilling to toe government line.
The shutting down of banks associated with the likes of Andrew Kimani Ngumba in the 1980s and the forced collapse of businesses of Mr Kenneth Matiba in 1990s come to mind.
In the end, it is the economy of the nation that is going to be crippled. It is the youth of our country who are going to suffer joblessness.
This emerging pattern must be nipped in the bud. Kenyans must stand firm and refuse to be blackmailed and intimidated.
I appeal to the Jubilee government to accept that Kenya is a multiparty state by law. That is not negotiable.
Let Jubilee accept that in a multiparty environment, we can disagree without being disagreeable.
Jubilee must put the interests of Kenya above self preservation.
A nation is in peril when all that the leaders do is plot and scheme how to subdue real or imaginary opponents.
Kenyans deserve an explanation on the closure of the two businesses associated with Governor Joho.
It is our understanding that the government should create jobs, not kill them.
We want an assurance in word and deed that the government shares this position.
HON RAILA ODINGA, EGH
JANUARY 29, 2016.

SOMA UJUMBE MUHIMU WA LEO

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI KUTOKA TANZANIA CLASSIC

$
0
0
                       ..
.
.
.
.
DSC00529
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC00558
.
DSC00560
.
DSC00563
.


Zitto Kabwe: "Serikali Imekurupuka, Kuongoza Nchi Siyo Kutumbua Majipu Tu"

$
0
0


Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kuonesha masikitiko yake kwa kitendo cha serikali kushindwa kuleta Bungeni mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano.
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi jambo ambalo serikali inapaswa kufanya baada ya uchaguzi na kusema ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
"Shughuli ya kwanza ya serikali baada ya uchaguzi ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ( kutafsiri ilani yake kwenda kwenye mpango wa utekelezaji) . Bunge linapaswa kujadili na kuidhinisha Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 na kisha Mpango wa mwaka mmoja kuanza kutekeleza Mpango huo wa miaka 5. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT Ibara ya 63(3)(c), Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 hutungiwa sheria kwa ajili ya utekelezaji." Alisema Zitto Kabwe
"Leo Serikali ya Rais John Magufuli ilipangiwa kuwasilisha Mpango huo wa Maendeleo wa miaka 5. Imeshindwa. Imeleta mwelekeo wa Mpango. Haikuleta sheria na Kamati ya Bajeti Imeleta maelezo yake kuhusu Mpango wa Maendeleo wa mwaka mmoja ilhali hakuna Mpango wa Miaka 5. 
"Mwenyekiti Chenge alitaka wabunge wajadili kwa mujibu wa kanuni ya 94 ambayo kimsingi ni Kanuni inayohusu Mpango wa mwaka mmoja. Serikali imejichanganya. Uongozi wa Bunge umechanganyikiwa." Aliongeza Zitto Kabwe
Zitto Kabwe alimaliza kwa kusema kuwa ni aibu kubwa kwa serikali inayojinasibu kwa kauli ya "Hapa kazi tu"
"Bunge linapaswa kuagiza Serikali ikalete Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 ili uidhinishwe na utungiwe Sheria kabla ya kuanza kujadili mipango ya mwaka mmoja mmoja.
"Ni aibu kubwa kwa Serikali ya ‪#‎HapaKaziTu‬ kushindwa kuleta Bungeni Mpango wake wa Maendeleo wa miaka 5 na hata ule wa mwaka wake wa kwanza. Itapangaje bajeti zake? Itatekeleza vipi ilani yake? Kuongoza nchi sio kutumbua majipu tu, ni kuendesha nchi." Alimaliza Zitto Kabwe.

.CHAGONJA ATEULIWA RAIS KUWA KATIBU TAWALA

$
0
0

Paul Chagonja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Balozi Sefue amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisiPaul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Aidha, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.
Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa kesho Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, saa nne asubuhi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
29 Januari, 2016

TAARIFA MUHIMU KUHUSU JENERALI MWAMUNYANGE KUONGEZEWA MUDA NA RAIS MAGUFULI KWENYE NAFASI YAKE

$
0
0

RAIS John Magufuli amemwongeza mda wa mwaka mmoja,Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Akizungumza na waandishi wa habari,leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi ya ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali wawili,  ambapo wote kwa  pamoja kwa pamoja wamestaa ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 31 Januari,2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 31 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,”amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo,imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo tena.
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi,

    Sanajari na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia,Rais Magufuli , amefanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo ili baada ya kuteua watu kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya jeshi hilo,
    Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais, ni Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa  kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu,ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria,ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.

Jeneral Mwamunyange alimtaja pia aliyeteuliwa na Rais,ni -Meja Jenerali-Yakub Sirakwi kuwa  Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) - kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii,Meja Jenerali Sirakwi alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.

Mwengine ni aliyeteliwa na Rais Magufuli ni -Brigedia Jenerali George William Ingram, kuwa  Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga, ambaye aliyechukua nafasi ya  Meja Jenerali Joseph  Pwani aliyestaafu leo kisheria baada ya kufikia umri wa kustaafu,Bregedua Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.

 Pia Rais Magufuli alimteua Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo  kuwa Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa-,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo, baada ya kufikisha umri wa kustaafu kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.

Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu  kuwa  mkuu wa shirika la mzinga-,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umrii,Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.

  Hata Hivyo,Rais Magufuli  amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjela, kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS)- kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi,baada ya kufikisha umri kustaafu kisheria,Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
   Aidha,Rais Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole kuwa   Kamanda wa Brigedia ya Tembo,- kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo baada kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu,Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa bAfusa Mnadhimu makao makuu wa Jeshii.
  Rais Magufulia pia amemteua  Bregedia Jenerali Sylevesta M.Mijna kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kzai leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria,ambapo kabya ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.
CHANZO:FULL  HABARI

Arsenal wanasajili hawa wawili kutoka Nigeria.

$
0
0
Screen Shot 2016-01-30 at 5.51.03 PM
picha imepigwa akiwemo kocha wa Arsenal, Nwankwo Kanu na wachezaji Nwakali na Samuel Chukwueze. Picha hiyo imepigwa kwenye ofisi za makao makuu ya club ya Arsenal ambapo wamekutanishwa na kocha huyo wakielekea ku-sign kwa ajili ya kucheza Arsenal.
Wote wawili wana umri wa miaka 17 na wamefuatiliwa na Arsenal wakati wa kombe la dunia la chini ya miaka 17 ilifanyika Chile. Wote wawili wanategemewa kuwekwa kwenye mpango wa vijana wa Arsenal ili kujiendeleza na kabla ya kujiunga na timu ya wakubwa.
Baadhi ya wachezaji waliopitia hatua kama hii ni Cesc Febregas ambae aliingia akiwa na miaka 15.
Screen Shot 2016-01-30 at 5.51.12 PM

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI KUTOKA TANZANIA CLASSIC

$
0
0
                                .DSC00579

DSC00580
Add caption
DSC00573DSC00574DSC00575DSC00576DSC00577DSC00578DSC00581DSC00582DSC00583

DSC00584DSC00585DSC00586DSC00587DSC00588DSC00589DSC00590DSC00591DSC00592DSC00593
DSC00594DSC00595DSC00596DSC00597DSC00598DSC00599DSC00600DSC00601DSC00603
Viewing all 5823 articles
Browse latest View live