Quantcast
Channel: TANZANIA CLASSIC
Viewing all 5823 articles
Browse latest View live

SOMA HAPA!!!! HUYU NI TERRY GOBANGA AMBAYE SIKU YA HARUSI YAKE ALITEKWA NA KUBAKWA NA WANAUME 3

$
0
0

KUTOKA KATIKA POST ZA NYUMA NILIZOWAHI KUANDIKA ZIKABAMBA
TERRY GOBANGA
Mmoja wa follower wangu alinitumia video ya huyo mama.Baada ya kuitazama nikafatilia kumjua zaidi story yake.
Huyo mama hapo juu ni kutoka nchini Kenya na kwa sasa ni pastor.Terry miaka 12 iliyopita siku ya harusi yake alitekwa na kubakwa na wanaume watatu.Wakati akitapa tapa mmoja wa wale wanaume alimchoma kisu cha tumbo na wakatumpa barabarani akiwa kapoteza fahamu kwenye dimbwi la damu.Akachukuliwa na gari ya polisi wakijua amekufa kumpeleka mochwari lakini alipokohoa wakamkimbiza hospitali kupata huduma.Eneo alilochomwa kisu baada ya oparation madokta walisema hataweza kuzaa maana kisu kilichoma kizazi.
Miezi nane baadae alipona na kufunga ndoa na mpenzi wake ambae aliishi nae kama mume kwa siku 29 tu.Mumewe alifariki usiku usingizini na usiku huo kabla ya kulala alimuuliza mkewe hivi nikifa leo utaishije?naona utapata tabu sana.Kifo kile cha mumewe kilimuhuzunisha sanaa na kuhisi Mungu anamuonea akaanza kuonyeshewa vidole na kupachikwa majina kuwa ananuksi.
Terry alipata faraja sana kwa kaka ambae sasa ni mumewe.Huyu alikuwa akimpa moyo na kumfariji na ndio alimpeleka kanisani.Baada ya miaka miwili wakapendana na baadae kufunga ndoa.Miaka yote aliishi akijua hapati mimba na hata mume huyu alimuoa alijua hilo na alikubali wataishi hivyo.Kama Mungu amepanga kuwapa watoto atawapa kama hakupanga basi.
Miezi kadhaa baadae akapata mimba madokta wakamwambia aitoe anaweza kufa akagoma akaibeba kwa shida na kujifungua mtoto wa kike.Na baadae tena akapata mimba ingine sasa hivi ana watoto wawili.Anamtukuza Mungu na kuhubiri neno lake kwa makubwa alomtendea.
Hii story nimeifupisha sana.
Nimekuletea wewe pia kwa ufupi ili kukupa moyo.MUNGU ndio anajua hatma yako na kila jaribu linalokutokea leo lina sababu.Unachekwa,unadharaulika,
unapewa majina ya kejeli na wanadamu.Sali,swali,soma dua,fanya maombi yeye pekee ndio atakuvusha.Na ipo siku utaheshimika,utasafishika na kung'aa kama dhahabu.
Barikiwa!
imeandikw na 

Picha leo!!!! Mhe Maalim Seif Shariff Hamad akimfariji mama mzazi wa marehem Bi:Asha Bakar ambaye alikuwa kada wa ccm

$
0
0

Aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi - CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, akimfariji mama mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakar Makame, alipoitembelea familia hiyo kwa ajili ya kuifariji, leo Jang'ombe, Zanzibar.

Picha na Hassan Hamad!

SOMA TAARIFA KUTOKA IKULU JUU YA RAIS MAGUFULI KUMTEUA MHE KIKWETE KUWA MKUU WA CHUO

Rais Magufuli: Mkuu wa Mkoa ambaye mkoa wake utakuwa na njaa atafukuzwa kazi

$
0
0


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli amesema kuanzaia sasa hataki kusikia malalamiko ya wananchi juu ya suala la njaa na ikitokea akasikia vilio hivyo vikiendelea mkuu wa mkoa husika atachukuliwa hatua ikiwemo ya kufukuzwa kazi.

Mh. Magufuli ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ameyasema hayo alipokuwa njiani kutoka jijini Arusha kwenda wilaya Monduli kwa ajili ya kufunga mazoezi ya kijeshi ya kuonyesha uwezo wa medani 2016 yaliyofanyika katika Briged ya 303 iliyoko Monduli.

Aidha Mh rais Dr. Magufuli amesema ni jambo halikubali kuendelea kusikia malalamiko ya wananchi juu ya mambo yaliyoko ndani ya uwezo na yanayoweza kutatuliwa na wakuu wa mikoa na ameendelea kuwataka viongozi na watendaji wa serikaali kutimiza wajibu ukiwemo wa kuwatumikia wananchi.

Kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya kero ya rushwa mh Rais amewataka wananchi hao kuwa wapole kwani kero itashughulikiwa na itapata ufumbuzi kwani zoezi la kutumbua majipu linaendelea na kwamba kinachofanyika sasa ni kutumbua majipu yaliyoiva ambayo ni sehemu ndogo tu ya majipu yaliyopo.

Membe atoa kauli , Apinga kufutwa uchaguzi wote Zanzibar,

$
0
0

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Waliohama CCM wananitia kichefuchefu

Membe pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM walioamua kutimkia upinzani wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu, akisema wanamchefua.

Akijibu swali lililotaka kujua anavyowazungumzia na kujisikia kuhusu watu hao, Membe alisema: “Nikionana nao najisikia kichefuchefu. Tena ukiwaona waambie, chama kichukue hatua kwa wasaliti.”

Alisema zipo taarifa za baadhi ya waliohama CCM kutaka kurejea, akashauri kisiwapokee tena.

“Nasikia wanataka kurudi, wasipokewe, hawa wasirudi,” alisema Membe ambaye alikuwa akichukuliwa kuwa mpinzani mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM.

Lowassa alihamia upinzani baada ya kuenguliwa na CCM na akapitishwa na Chadema kugombea urais.


Chanzo: Mwananchi

SOMA TAMKO KALI LA CUF BAADA YA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR KUTANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI

$
0
0


Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam.

Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO

Must read!!! To WIN in 2017 Raila may NEED a few strategic persons in Mt Kenya and Rift Valley- Hon Wafula Buke

$
0
0

ODM director for Strategy and Political affairs Wafula Buke has told off supporters of CORD Leader Raila Odinga opposed to the party/campaign secretariat working closely with individuals from Mt Kenya and Rift Valley.
Buke said the Odinga secretariat will benefit directly or indirectly from individuals from two the regions perceived to be Jubilee strongholds.
Such persons whether they are moles, spies, Judas, traitors or whatever you want to call them will definitely offer some valuable input, its the secretariat and party leader to judge to what level of responsibility such individuals should be trusted with BUT not a blanket condemnation and isolation- I can tell you the Ngunjiri Wambogos gave a lot of actionable informationanother ODM insider hinted.
Here is the post by Buke that caught some ODM ‘extremists’ by surprise;
”Learn from baba!! we won our first election 2007 because we had so much energy and information from the enemy camp (franklin bet, sally kosgey etc.
Museveni commandeered the first take over by a guerrilla movement in 1986 because he had the benefit of having been in the Obote administration and many defectors from the Obote army such as the FERA boss brig. Odongo.
Gacoka is a political windfall more useful to us than a number of us courtesy of his reach. Baba is greater than you imagine. Euro bond infor? NYS deals? No sycophancy people. expect more of the same”
– Wafula Buke
Buke was reacting to harsh comements by ODM extrimists that called on Raila to ignore advances by Tony Gachoka who seem to be keen to join the ODM brigade. Gachoka has previously worked for Odinga and also as a close ally of Water minister Charity Ngilu (Mrs Ngilu was dumped by Uhuru on allegation of corruption).

MAN UTD YAKWAMA TENA OLD TRAFFORD

$
0
0

United vs South 2
Klabu ya Manchester United imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kujikuta ikigaragazwa kwa bao 1-0 dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
United vs South 3
Ilimchukua dakika saba na sekunde 43 tu, Charlie Austin kuiandikia bao Southampton akitokea benchi dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Mane. Austin aliweka mpira wavuni dakika ya 87 akiunganisha kwa kichwa krosi ya James Ward-Prowse na kuipa ushindi timu yake ikiwa kwenye uwanja wa ugenini.
United vs South 5
Kipigo cha leo kinaifanya Man United kuendelea kubaki nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi, ikiwa na point 37 katika michezo 23. Huo ni mchezo 6 kwa Man United kupoteza toka kuanza kwa msimu wa 2015/2016.
United vs South 4
Vikosi vya timu zote vilivyocheza mchezo wa leo Manchester United vs Southampton
United vs South
Takwimu za mchezo kati ya Manchester United vs Southampton
United vs South 1
Matokeo ya mechi nyingine za EPL zilizopigwa leo Jumamosi January 23
Norwich 4-5 Liverpool
Crystal Palace 1-3 Tottenham
Leicester City 3-0 Stoke City
Man Utd 0-1 Southampton
Sunderland 1-1 Bournemouth
 Watford 2-1 Newcastle Utd
West Brom 0-0 Aston Villa
Video ya goli la Charlie Austin dhidi ya Manchester United

LIVERPOOL YAPATA POINTI 3 UGENINI, LAKINI YAKIONA CHA MOTO

$
0
0

Lalana
Adam Lalana amewatoa Liverpool kimasomaso baada ya kuifungia timu hiyo bao la ushindi dakika za lala salama kwenye mechi ya ligi kuu England kati ya Norwich City dhidi ya Liverpool iliyomalizika kwa magoli tisa (9) kufungwa kwenye game hiyo.
Lalana 5
Roberto Firmino alianza kuweka kambani bao la kwanza kuiweka Liverpool mbele ya Norwich kabla ya Dieumerci Mbokani kuisawazishia Norwich kwa bao la kisigino.
Lalana 3
Steven Naismith akapachika bao la pili na kuifanya Norwich kuongoza kwa bao 2-1 hadi mapumziko.
Lalana 4
Wes Hoolahan akaongeza goli la tatu kwa mkwaju wa panati upande wa Norwich dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Jordan Henderson na Firmino kupiga mabao na kuufanya mchezo huo kuwa sawa kwa magoli 3-3.
Lalana 2
James Milner akatupia bao jingine na kuifanya Liverpool kuwa mbele kwa bao 4-3. Sebastian Bassong aliifungia Norwich bao la kusawazisha zikiwa ni dakika za nyongeza lakini bao hilo halikudumu baada ya Lalana kuipa Liverpool ushindi wa ugenini kwa kufunga bao la tano na kufanya matokeo yasomeke Norwich 4-5 Liverpool.
Lalana 1,

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI KUTOKA TANZANIA CLASSIC

VIJANA WASOMI 'WAVUA NGUO' HADHARANI BERNAD MEMBE..... NI BAADA YA KUMKOSOA MAGUFULI KWA KUTOSAFIRI NJE YA NCHI.

$
0
0

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa kuelezea masikitiko makubwa kutokana na kauli za hivi karibuni za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndugu Bernard Membe. Akifanya mahojiano na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 22 na 23 Januari, 2016 , ndugu Membe amekaririwa akitoa kauli zenye maudhui ya kubeza juhudi za mh. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Kauli hizi zilijikita katika maeneo makubwa manne kama ifuatavyo:-

1. Ndugu Membe  amebeza juhudi za Rais Dr. John Magufuli za kupunguza ukubwa wa serikali, na kwamba hatua yake ya kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri haijasaidia chochote kwa taifa. Na kwamba ni sawa na kupunguza idadi ya mifuko huku idadi ya mayai ikiwa ni ile ile.

2. Ndugu Membe amekosoa na kubeza hatua ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. Magufuli ya kupunguza safari za nje zisizo za lazima na tija kwa taifa, na kwamba safari hizo zilikua na neema kubwa kwa watanzania.
3. Ndugu Membe amepinga kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar na kudai kwamba dunia nzima inatushangaa kwa uamuzi huo.

4. Ndugu Membe amekosoa mazungumzo ya kutafuta maridhiano baina ya Chama cha CUF na CCM visiwani Zanzibar huku akidai kuwa ni makosa kuwaachia Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein na Maalim Seif Shariff  Hamad kufanya mazungumzo peke yao.
Tumesikitishwa sana na kauli hizo na vijana wasomi tumeamua kumjibu kama ifuatavyo:-

KUPUNGUZA UKUBWA WA SERIKALI
Rais Dr. John Magufuli amechukua juhudi za kupunguza ukubwa wa serikali kwa kuanza na baraza la mawaziri. Idadi ya mawaziri imepungua kutoka mawaziri 60 wakati wa serikali ya awamu ya nne hadi mawaziri 34 tu katika serikali ya awamu ya tano. Punguzo hili ni idadi ya mawaziri 26.

Gharama za kawaida za kumuhudumia waziri zilizopungua:

a. Kila waziri na naibu wake hupewa gari aina ya GX V8 ambalo thamani yake inakadiriwa milioni 400. Gari hili linahitaji  mafuta na gharama ya kulitunza. Hivyo magari 26 yamepungua ambayo gharama yake ya manunuzi na matunzo ni mabilioni ya pesa.

b. Nyumba ya kuishi. Mawaziri wote wanapewa nyumba na serikali. Nyumba hizo zinalipiwa umeme na maji

c. Wasaidizi wa mawaziri. Kila waziri anapewa katibu wake, hivyo serikali imepunguza nafasi 26 za makatibu kwa kupunguza mawaziri 26. Hawa wanalipwa mishahara na posho.

d. Madereva. Kila waziri ana dereva wa serikali anayelipwa mshahara na posho awapo nje ya kituo cha kazi. Hivyo serikali imepunguza mishahara na posho za watu 26.

e. Kila waziri anapewa ulinzi nyumbani kwake wa askari wawili wa jeshi la polisi masaa 24. Hivyo kwa kupunguza mawaziri 26, tumepunguza askari 52 ambao sasa watakwenda kuongeza ulinzi wa raia na mali za wananchi wengine.

f. Kila waziri anatengewa mafungu ya fedha kwa ajili ya mawasiliano, safari zake za kikazi, ziara za mikoani, vikao na majukumu mengine ya kazi ambayo ni mamilioni ya shilingi kila mwezi. Kwa kupunguza mawaziri 26 Rais ameokoa mamilioni ya shilingi kila mwezi.

g. Gharama za kuwahudumia mawaziri 26 wakiwa bungeni Dodoma pia zimepungua.

 WIZARA ZILIZOUNGANISHWA
Katika muundo wa baraza la mawaziri la Dr. John Pombe Magufuli alilolitangaza , ziko wizara 5 ambazozimeunganishwa pamoja. Wizara hizi ni
a. Kilimo, Mifugo na Uvuvi (wizara 3 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)-Mh. Mwigulu Nchemba
b. Wizara ya mambo ya nje, kikanda na kimataifa (wizara mbili zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)- Mh. Augustine Mahiga
c. Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji (wizara 2 zimeunganishwa,sasa zina waziri 1)- Mh. Charles Mwijage
d. Wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi (wizara 2 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)- Mh. Joyce Ndalichako
e. Wizara ya ujenzi, mawasiliano na Uchukuzi (wizara 3 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1) -Mh. Makame Mbarawa

Katika hali hiyo, ni dhahiri idadi ya mawaziri imepungua na hivyo gharama ya kuwahudumia pia imepungua. Kutoka hadharani na kusema hakuna kilichopungua ni upotoshaji mkubwa ambao mtu mwenye uelewa wa kawaida kabisa anaweza kuubaini.


IDADI YA MAKATIBU WAKUU
Makatibu wakuu na manaibu waliohudumu wizara wakati wa serikaliya awamu ya nne walikua jumla ni 54. Mh. Rais Dr. Magufuli ameteua makatibu wakuu 29 na manaibu 21. Hivyo hapa pia idadi imepungua na kufanya gharama kupungua pia.

WATANZANIA WANAMSHANGAA MEMBE
Kitendo cha ndugu Bernard Membe kudai kuwa kupungua huku kwa ukubwa wa baraza la mawaziri hakujasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, ni jambo la ajabu ambalo watanzania wote wanalishangaa na kuliona kuwa ni uongo na upotoshaji mkubwa. Upotoshaji huu unastahili kupuuzwa na kila mpenda mabadiliko ya kweli.
Baada ya Mh. Raisi kuteua baraza lake la mawaziri mwezi desemba, mwanazuoni profesa Samuel Wangwe alikaririwa na gazetila Habari Leo la tarehe 11 Desemba, 2016 akisifu Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kupunguza idadi ya mawaziri. 

Profesa Wangwe alisema mawaziri ni watu wa kusimamia sera, na watendaji wakubwa ni makatibu wakuu. Aidha, wanaharakati na wadau mbalimbali wote walipongeza kupunguzwa huko kwa baraza la mawaziri wakisema taifa limepunguza mzigo. Lakini ajabu, ndugu Bernard Membe hajaliona hilo. Inasikitisha sana.

Wakati mwingine inatufanya tujiulize, ndugu Membe ambaye alikua miongoni mwa wana CCM waliowania kuteuliwa na Chama kugombea Urais wa Tanzania, na baadae kushindwa kwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, amesema maneno haya kwa malengo au makusudio yapi? Waswahili wanasema, aliyepata kapata. Tunamtaka ndugu Membe ajiunge na watanzania kukubali kuwa Dr. Magufuli ndiye Rais wa nchi yetu aliyechaguliwa na wananchi. Hivyo amuache atimize wajibu wake kwa taifa.

KUPUNGUZA SAFARI ZA NJE
Katika hatua nyingine ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini, Raisi ameagiza kufutwa kwa safari zote zisizo za tija kwa nchi, na kwamba safari zote zitatolewa kwa kibali maalum cha Raisi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli bungeni mjini Dodoma, safari za nje za miaka miwili pekee (2013-2015) ndugu Membe akiwa waziri wa mambo ya nje, shilingi bilioni 356.324 zilitumika kwa safari za nje huku tiketi za ndege peke yake zikigharimu bilioni 183.160. 

Taasisi zilizoongoza kwa matumizi hayo ni pamoja na wizara ya mambo ya nje aliyokuwa anaihudumia ndugu Membe. Tunajiuliza, ni trilioni ngapi zilitumika kwa safari za nje katika kipindi chote cha miaka 8 ambacho ndugu Membe alikuwa waziri? Je, huu haukua mzigo kwa taifa? Ndugu Membe anazungumziaje matumizi haya mabovu ambayo yalifanyika yeye akiwa na dhamana ya wizara hiyo?
Watanzania wote tunafahamu na kukubali kuwa safari hizi zilikua mzigo mkubwa kwa taifa, na tunaunga mkono juhudi za kupunguza na kudhibiti safari zisizo za lazima.

 BERNARD MEMBE SI MKWELI
Ndugu waandishi, ili kudhihirisha kuwa ndugu Bernard Membe si mkweli kwa anayoyasema kuhusu safari za nje, na kwamba kauli zake kuhusu jambo hili zinakinzana, baada ya hotuba ya Rais Dr. John Magufuli bungeni mjini Dodoma, bwana Membe alinukuliwa akimpongeza mh Rais kwa uamuzi wake wa kupunguza safari za nje kwani kwa maneno yake alisema walikua wanapishana angani kama vile nyumbani kunawaka moto.

Ni Bernard Membe huyuhuyu ambaye leo anatafuna maneno yake bila aibu na kutueleza kuwa safari zile zilikua na neema kwa taifa.

KUHUSU KUTOKUA NA BALOZI KATIKA NCHI ZOTE
Katika kuhalalisha safari za nje zisizo za lazima, ndugu Membe alieleza kuwa Tanzania ina mabalozi 36 tu katika nchi 194 ambazo tunapaswa kuwa na mabalozi.

Tunapenda kumfahamisha ndugu Membe kuwa kutokuwa na balozi katika nchi zote sio kigezo cha kutumia mabilioni ya pesa kwa ajili ya safari zisizo na tija kwa taifa. Kutokana na kuwa uchumi wetu bado unakua, na haustahamili gharama za kuweka mabalozi katika nchi zote, wako mabalozi wetu nje ya nchi ambao wanawakilisha nchi zaidi ya moja zilizoko katika ukanda mmoja. Mfano, balozi Ombeni Sefue aliwahi kuwa balozi wetu Marekani akiwakilisha pia CUBA. Aidha, uamuzi wa nchi kufungua ubalozi katika nchi nyingine hutegemea vigezo mbalimbali kama faida za kiuchumi, kisiasa, kiusalama na kidiplomasia.

RAISI HAJAKATAA KUSAFIRI NJE YA NCHI
Ndugu Membe anapotosha ukweli anaposema Tanzania sio kisiwa na kwamba Raisi na waziri wake wa mambo ya nje lazima wasafiri nje ya nchi watake wasitake.

Tunapenda kumfahamisha ndugu Membe kuwa, mh. Raisi Dr. John Magufuli hajatoa kauli kuwa yeye au wasaidizi wake hawatosafiri nje ya nchi katika safari za muhimu na zenye tija. Isipokuwa, muongozo wa mh. Rais kuhusu safari za nje unalenga kupunguza safari zile ambazo hazina ulazima na tija kwa taifa.

KUHUSU MGOGORO WA UCHAGUZI WA ZANZIBAR

Katika maelezo aliyonukuliwa na gazeti la Mwananchi, ndugu Membe alieleza kupinga kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi wa Zanzibar yakiwemo ya wawakilishi, na kwamba jambo hili limeihuzunisha dunia.
Kauli hii ya ndugu Membe inatushangaza na kutusikitisha sana. Kwanza tunajiuliza, Je, ikiwa sehemu kubwa ya uchaguzi iligubikwa na udanganyifu na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kinyume na sheria za uchaguzi wa Zanzibar, ni kwanini ndugu Membe ashangae uchaguzi wote  kufutwa na tume ya uchaguzi ZEC?
Tunamtaka ndugu Membe atueleze, ni dunia ipi hiyo inayotushangaa?
Ni kwanini dunia hiyo anayoitetea ndugu Membe haijashangaa kumuona maalim Seif Shariff Hamad akijitangaza kuwa mshindi kinyume cha sheria za uchaguzi?
Ndugu Membe anapaswa kushangaa, ni kwanini hadi leo hii maalim Seif Shariff Hamad hajakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kujitangaza kuwa mshindi kinyume cha sheria.

KUHUSU VIKAO VYA MARIDHIANO
Kuhusu vikao vya maridhiano vilivyokua vinaendelea, ndugu Membe amekosoa kitendo cha Raisi wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na maalim Seif Shariff hamad kuachwa wakazungumza wenyewe wawili.
Kwanza tunasikitika kuwa ndugu Membe huenda ama hajui kinachoendelea Zanzibar au ameamua kupotosha umma kwa makusudi. Hii ni kwasababu mazungumzo yaliyokua yakiendelea Zanzibar, hayakuwahusisha Dr. Shein na maalim Seif Shariff peke yao. Bali yalishirikisha marais wastaafu wa Zanzibar, Raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar.
Pili, katika muafaka wa kisiasa wa Zanzibar wa mwaka 2009/2010 uliopelekea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kwa kiasi kikubwa ni maalim Seif Shariff hamad na Rais wa Zanzibar wa wakati huo mh. Amani Abeid Karume pekee walioshiriki mazungumzo.

RAI KWA NDUGU MEMBE
Mosi, tunapenda kumkumbusha ndugu Bernard Membe kuwa yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa amewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM. Hivyo anajua utaratibu wa Chama na anayo nafasi ya kuyasema mawazo yake juu ya uendeshaji wa serikali ndani ya vikao halali vya chama. Aidha, ndugu Membe kwa nafasi yake kama mjumbe wa NEC na waziri wa zamani wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,  anayo nafasi ya kutoa ushauri na maoni yake moja kwa moja kwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Dr. John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM taifa Dr. Jakaya Kikwete au kwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.
Kutotumia fursa hizo kutoa maoni yake ni kujishushia heshima mbele ya jamii. 

Pili, tunamkumbusha ndugu Membe kuwa yeye sasa ni mstaafu aliyeitumikia nchi yake kwa muda mrefu na nafasi mbalimbali. Ni vema sasa akatoa fursa kwa viongozi wengine walioko madarakani kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia watanzania. Muda wake umekwisha na sasa ni busara akakaa kimya na kuchunga maneno yake.
Raisi mstaafu wa awamu ya tatu mh. Benjamin William Mkapa aliwahi kusema (nanukuu):-
"Siku moja mtoto mdogo aliwahi kuniuliza. Nani ni bingwa wa kuendesha shughuli za serikali? Nikatafakati sana swali lile, kisha baada ya muda nikamjibu…Ni mwanasiasa aliyestaafu kisha akachunga ulimi wake…"
MWISHO

Tunamshauri ndugu Membe kuuchukua ushauri huu wa Raisi mstaafu Benjamin Mkapa, utamsaidia. Aidha tunamtaka afahamu kwamba watanzania wana imani kubwa na juhudi zinazofanywa na serikali katika kupunguza matumizi, kuziba mianya ya rushwa, ukwepaji kodi na ubadhirifu wa mali za umma. Wakati huu si wa kupika majungu, fitina wala ubabaishaji. Ni wakati wa kuungana pamoja kama taifa na kuchapa kazi tu.
Asanteni.

Imetolewa na ndugu
ALLY S. HAPI
KATIBU WA IDARA,
ELIMU, UTAFITI NA UONGOZI,

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA

Wanachama wa CHADEMA Wamvaa Benard Membe Baada ya Kusema Hujisikia Kichefuchefu Akionana na Makada Walioihama CCM

$
0
0
Bernard Membe

Siku moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kusema akionana na waliokuwa wanachama wa CCM na kuhamia upinzani anajisikia kichefuchefu, waliokuwa makada wa chama hicho wamemshukia kwa kauli yake hiyo.

Membe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akitoa maoni yake kuhusu makada waliohama na kusisitiza kuwa wasipokewe endapo watataka kurudi.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye alitimkia Chadema, alisema kama angesikia maneno hayo kwa mtu mwingine asingeshangaa, lakini siyo kwa Membe.

Mbunge huyo wa zamani wa Arumeru – Magharibi, alisema Membe anapata masilahi yake kwa kutambulika kama waziri mstaafu na wakati anaapa kuwa katika nafasi hiyo alitumia Katiba ambayo hivi sasa kwa kupinga yaliyomo ikiwamo uhuru wa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, anakosea.

Medeye alisema kwa kauli hiyo, Membe hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya siasa kwa sababu haamini katika vyama vingi wakati Taifa linaendeshwa kwa Katiba inayokubali suala hilo.

Alisema hata kauli ya Membe ya kutounga mkono uchaguzi kurudiwa Zanzibar akitaka kufanyiwa kazi kasoro chache ni ya kinafiki kwa sababu ameonyesha kutopenda upinzani.

“Hana msimamo hazungumzi vitu kutoka moyoni, kama kweli anakubali vyama vingi na ana uchungu na kinachoendelea Zanzibar, kwa kuwa bado ni mjumbe wa Nec (Halmashauri Kuu ya CCM), angemuomba mwenyekiti wake aitishe mkutano mkuu lijadiliwe hilo na atoe anachokiamini, hakufanya hivyo kwa sababu hakubali vyama vingi, hataki mabadiliko katika siasa anayoitumikia, ” alisema Medeye.

Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alisema hawezi kujibizana na watu kwani anajua anachofanya.

Alisema anayo mawazo huru na akitaka kuzungumza jambo lolote atafanya hivyo kwa utashi wake na siyo kujibizana na watu waliozungumza kwa utashi wao.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita alisema anamheshimu Membe kwa sababu amefanya naye kazi katika chama hicho tawala na kumshauri siku nyingine anapozungumza mambo kama hayo asiegemee upande mmoja.

Alisema licha ya kuwa hayo ni mawazo yake na kila mtu ana uhuru wa kuwaza na kusema anachotaka, alipaswa apime anazungumza nini na kwa manufaa ya nani.

Guninita alisema Katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama hata mara 10 alimradi huko anakokwenda atapata vitu muhimu ikiwamo malengo yake binafsi, ya chama husika na mafanikio ya Taifa.

Alisema haikuandikwa ni lazima abaki sehemu anayoamini hana malengo nayo, au asihame kutoka chama kimoja ama kingine

Mrembo wa UDSM Aliyedaiwa kuwa Msukule Uliokutwa Kwenye Shimo la Mfanyabiashara Dar Anena kwa Uchungu

$
0
0

Picha zinazomuonesha mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya kutisha zimetumiwa kufanya upotoshaji kwa kumzushia msichana mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Picha iliyounganishwa ikionesha taswira ya msichana huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakidai kuwa hapo ni kabla zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema na kusababisha usumbufu kwa mrembo huyo.

Msichana huyo ambaye anatumia jina la Ms.Adelaide kwenye Instagram amekanusha vikali taarifa hizo huku akieleza kwa uchungu jinsi ambavyo ameathiriwa na uzushi huo.

“NAJUA WENGI MTAKUA MMEKUTANA NA HIZI HABARI..SIJAJUA NANI ALIEANZISHA HII MADA NA SIJUI IMEANZIA KWA NANI.
 "MIMI NI MZIMA NA SIO MSUKULE JAMANI NINA WAZAZI WOTE WAWILI WAPO HAI NA WAMEUMIZWA SANA NA HIKI KITENDO, MY FAMILY MEMBERS WAMEUMIA MNOOO KUPITA KIASI
"LICHA YA HIYO MIMI BADO NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, WANAFUNZI WENZANGU WENYE MAPENZI NA MIMI WANAUMIA SANA PIA WANAPOONA MAMBO KAMA HAYA. 
"PLEASE ACHENI KUENDELEZA HIZI HABARI ZA UONGO, TUSIPELEKANE MPAKA TCRA SASA MAANA TUTAKUA TUNAPOTEZEANA MUDA,” aliandika Instagram.

HII NDIO TOP 20 YA WANASOKA WENYE THAMANI ZAIDI DUNIANI 2016

$
0
0
Notes
  1. Paul Dybala $68.28m DybalaHaishangazi kumuona kinda huyu mwenye kipaji katika orodha ya wachezaji 20 wenye thamani kubwa zaidi hivi sasa, Juventus inajivunia kijana huyu na hawapo tayari kumuuza hivi sasa kutokana na uwezo wake wa kucheza sehemu yeyote katika mstari wa mbele wa ushambulizi.
  1. Diego Costa $71.56m Diego-Costa-Chelsea2Mshambuliaji huyu wa Chelsea amekua hana msimu mzuri tangu kuanza kwa msimu huu lakini fomu yake ya mwaka jana inamfanya aingie katika orodha hii ya wachezaji 20 wenye thamani kubwa.
  1. Romelu Lukaku $74.51m LukakuInakupa maswali mengi kwanini kocha Jose Mourinho alimuachia kijana huyu raia wa Ubelgiji mwenye miaka 22. Lukaku ameendelea kuzifumania nyavu akiwa na klabu ya Everton na hivi sasa anaongoza katika kinyang’anyiro cha ufungaji mabao nchini England.
  1. Gareth Bale $75.49m baleMajeruhi yanayomuandama mchezaji huyu huenda yamechangia kuwa pamoja na kuwa ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa gharama kubwa zaidi duniani, lakini thamani yake imepungua sana hadi sasa anashika nafasi ya 17. Anahitaji kupandisha gemu yake huku akibakia free injury ili arudi katika ubora wake.
  1. Robert Lewandowski $76.03m RobertRekodi yake ya mabao akiwa na Bayern Munich msimu huu na uliopita unamfanya Mpoland huyu kuwa mshambuliaji hatari zaidi wa kati duniani.
  1. Thomas Muller $77.89m MullerHuyu ni pacha wa Robert Lewandowski katika safu ya ushambuliaji, rekodi zake za mabao akiwa Bayern na timu ya taifa ya Ujerumani inamfanya Muller kuwemo katika orodha hii.
14. Philippe Coutinho $79.75m Coutinho 1Huyu bila shaka ni mchezaji Liverpool wanajivunia zaidi kuwepo katika kikosi chao hivi sasa. Amekua akifunga mabao muhimu sana, Liverpool wanahitaji kumshikiria mchezaji huyu kwani anaweza kushawishika kuihama klabu hiyo siku za usoni.
  1. Kevin de Bruyne $79.75m DE Bruyne UEFAKama ilivyo kwa Mbrazil Philippe Coutinho, Kevin de Bruyne ni moja ya wachezaji hatari zaidi katika mstari wa pili nyuma ya mshabuliaji. Haikua kazi kwa Manchester City kuilipa Wolfsburg pauni 54m kumnasa mbelgiji huyu.
  1. Paul Pogba 84.45m Paul PogbaKiungo huyu wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, alitajwa katika kikosi cha wachezaji 11 bora duniani pamoja na akina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo wanaozivutia klabu nyingi sana hivi sasa.
11. Anthony Martial $84.99m 
during the UEFA Champions League Group B match between Manchester United FC and VfL Wolfsburg at Old Trafford on September 30, 2015 in Manchester, United Kingdom.
Usajili wake kujiunga na Manchester United tena kwa pesa nyingi zaidi akiwa na umri wa miaka 19 tu, ulitajwa na wengi kama kamali, kijana huyu hivi sasa, pamoja na United kutokua na msimu mzuri, Martial anaonesha kuwa msaada mkubwa Old Trafford.
  1. Alexis Sanchez $89.47m Sanchez 5Huwezi kuwataja wachezaji watatu muhimu zaidi katika kikosi cha Arsenal ukamuacha Alexis Sanchez. Raia huyu wa Chile anastahili kuwa katika orodha hii.
  1. Sergio Aguero $89.69m agueroAnaweza kuwa ndiye mchezaji bora zaidi wa muda wote wa klabu ya Manchester City, ana kila kitu mshambuliaji anastahili kuwa nacho.
  1. Luis Suarez $94.28m Luis SuarezUmoja wake na Lionel Messi, pamoja na Neymar katika kikosi cha Fc Barcelona, unamfanya Suarez kuwa miongoni mwa wachezaji wenye thamani kubwa zaidi hivi sasa.
  1. Antoine Griezmann $96.46m Antoine-GriezmannBaada ya kuondoka kwa mastaa kadhaa kikosini Atletico Madrid, Mfaransa huyu anabakia kuwa tegemezi zaidi huku akifunga magoli karibu kila mechi.
  1. Raheem Sterling $98.10m raheem-sterlings-individual-high-1024x576Ugumu wa usajili wake kutoka Liverpool, sanjari na pesa waliyoitoa Manchester City unaonesha thamani halisi ya Raheem.
  1. Harry Kane $99.74m Harry Kane 2Ukitaka kujua thamani halisi ya kijana huyu mwingereza, ni pale utakapoamua kutaka kumsajili, ana kila kitu mshambuliaji anatakiwa kuwa nacho.
  1. Cristiano Ronaldo $124.54m 2D021C3500000578-3257538-Ronaldo_plants_a_kiss_on_the_boot_which_sits_on_a_base_reading_C-a-23_1443788956535Amemaliza kila kitu, umri unasogea, moja kati ya wachezaji bora zaidi kuibariki dunia ya mpira.
  1. Eden Hazard $142.56m Eden HazardWengi tunaweza kushtushwa na jina la Hazard katika nafasi ya tatu, lakini tukumbuke kuwa thamani ya mchezaji inahusisha vitu vingi sanjari na uwezo uwanjani, lakini pia mauzo ya jezi n.k
  1. Neymar $166.82m Neymar (1)Alibakia katika kinyang’anyiro cha wachezaji 3 waliokua wakiwania tuzo ya Ballon d’Or msimu huu, taa ya kijani imewaka kwa mbrazil huyu, anastahili kuwemo katika nafasi hii.
  1. Lionel Messi $273.84m lionel-messi-barcelona-la-liga3248555-1425893997-2343424Haihitaji maswali kwa kijana huyu mchawi wa soka, ni mchezaji ambaye dunia ina bahati kumshuhudia, ana kila kitu, hana mbadala, Ballon d’Or 5, sio kitu cha kawaida.

MBUNGE WA CCM BW: HUSSEIN BASHE AMSHAMBULIA MHE MEMBE KWA MANENO MAZITO,AMTAKA AMUACHE MAGUFULI

$
0
0
MHE  HUSSEIN  BASHE  AMBAYE  NI  MBUNGE  WA  CCM  CHINI  NI  KAULI YAKE KUPITIA UKURASA  WAKE  WA  FACEBOOK.
Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.
Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.
Hoja kuwa serikali haijapungua ama kubwa or ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .
Membe amekua sehem ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa,Amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi,Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake Magufuli believes matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya Hovyo na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.
Ni muhimu membe afahamu magufuli ana style yake tutampima kwx matokeo as of now hatujaona athari za safari labda membe kama yy binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kuli muathiri yy binafsi kwakukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Common wealth thats why leo anakosoa.
Tunafaham maamuzi mengi ya magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka ktk Awamu ya nne,Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.
Hoja ya kutokua na mabalozi magufuli hana siku 100 yy amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwx na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .
amekua mmoja wa mawaziri walouwa foreign relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu yx mis use of funds ktk wizara yake,kipindi chake safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.
Nimuhimu membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika ameathiriki directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari za nje.
Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya magufuli ya uongozi aliwahi kusema Sankara " You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"
Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu,wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wx kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha aliekuwa akinyonywa hapo awali tutasikia watu wa aina ya membe wengi kwakua style ya magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.
Wassalaam.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU KUTOKA TANZANIA CLASSIC

$
0
0
                           ;DSC00348
DSC00295
DSC00296
DSC00297
DSC00298
DSC00299
DSC00300
DSC00301
DSC00302
DSC00303
 DSC00305 DSC00306 DSC00307 DSC00308 DSC00309 DSC00310
DSC00322 DSC00323 DSC00324 DSC00325 DSC00326 DSC00327 DSC00328 DSC00329 DSC00330
DSC00340 DSC00341 DSC00342 DSC00343 DSC00344 DSC00345 DSC00346 DSC00347 DSC00348 

waziri mkuu wa zamani Dr Salim A. Salim ametaka haki itendeke Zanzibar kwa kumtangaza mshindi wa uchaguzi na si kurudia uchaguzi kama ilivyotangazwa na ZEC..

$
0
0

Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo.
Amesema jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo, amesema kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema.
Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana.  Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi  wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza  wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao. “Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutwa kumewashangaza wengi na bado suala hili halieleweki. “Pia hili jambo sidhani kama ni la mtu mmoja…sidhani kama ni la Jecha peke yake. Huu si mustakabali mzuri kabisa, Zanzibar ni nchi ndogo, lakini ina historia kubwa kisiasa hivyo juhudi za pamoja zifanyike kutatua mgogoro huu kwa matakwa ya Watanzania kwa ujumla.

Raila ‘hires’ former Russian SPECIAL FORCES RETIRED COMMANDOS as personal bodyguards

$
0
0

Raila ‘hires’ former Russian SPECIAL FORCES RETIRED COMMANDOS as personal bodyguards
Opposition chief Raila Odinga has hired 15 highly trained top notched former Russian SPETSNAZ, SPECIAL FORCES RETIRED COMMANDOS to guard him ahead of the highly anticipated 2017 polls.
According to our Russian counterparts, the Prime Minister went for the recently retired unmatched SPETSNAZ ALPHA Squad, only comparable to America’s Special Weapons And Tactics (SWAT) and the US MARINES.
The SPETSNAZ have the ability enter any country or highly secured buildings with or without permission. They are proficient in artillery and can operate any kind of ARSENAL however complicated.
They have the ability to operate any sophisticated gun including the prestigious General Multi-purpose Machine Gun (GPMG) and long-range missile and rocket launcher.
Raila’s team of the newly hired bodyguard can detect a criminal by looking at him, can read any criminal’s mind, can smoke out criminals from any hideout can fly any military aircraft, can pilot any warship including complicated submarines.
Among Raila’s new bodyguards are the 5 SPETSNAZ commandos that killed the Chechen terrorists during the 2002 Moscow theatre hostage crisis.
The commandos are scheduled to secretly land in the country soon and take their new assignment. The ‘government’ has approved the work permits for the special team however some Statehouse operatives are at crossroads because the SPETSNAZ are a million times super trained compared to those that are picked from academic failures with grade D perchance, taken to barracks, taught how to hold a gun and shoot, and graduated as soldiers and sent on a mission immediately.

SOMA MAGAZETI YA LEO KUTOKA TANZANIA CLASSIC

$
0
0
,
 DSC00413 DSC00392 DSC00394 DSC00395 DSC00396 DSC00398 DSC00400 DSC00402
DSC00403 DSC00404 DSC00405 DSC00406 DSC00407 DSC00408 DSC00409 DSC00410
DSC00411 DSC00413 DSC00414 DSC00415 DSC00416 DSC00417 DSC00418
DSC00419 DSC00420 DSC00421 DSC00422 DSC00423 DSC00424 DSC00425 DSC00426
,

SOMA UJUMBE WA LEO

Viewing all 5823 articles
Browse latest View live